Formula Za Kumtumia Mwanamke SMS ili Aweze Kukujibu

Formula Za Kumtumia Mwanamke SMS ili Aweze Kukujibu Kupokea jibu kutoka kwa mwanamke wakati mwingine si rahisi. Wanawake ni viumbe ambao hawatabiriki kirahisi. Anaweza akajibu jumbe zako na mara ghafla unapata kuona amekujeukia na hajibu meseji zako tena. Mara nyingi ukiona hatua kama hii fahamu ya kuwa amepoteza hamu na wewe na itakuwa vigumu kwake kuweza kuongea na wewe tena. Nakumbuka hivi juzi kabla janga hili la Corona Virus na karantini kutujia, niliweza kupewa namba na mwanamke niliyekutana naye mtaani. Kama kawaida nilijua ya kuwa itakuwa rahisi kwangu kuweza kumteka mwanamke huyu bila wasiwasi. Baada ya siku mbili ya kutumiana jumbe kwa chat, niliona amepunguza mazungumzo yake na mwisho kabisa akaacha kuchat na mimi. Ilikuwa pigo kwangu kwa kuwa haijakuwa jambo la kawaida kuweza kushindwa kuchat na mwanamke. Lakini uzuri juzi, wakati karantini imeanza na kila mtu amelazimishwa kukaa nyumbani kwa wale ambao hawana mishe mijini, alianza kunijibu yeye mwenyewe. ...